Kumbukumbu la Sheria 4:41-42
Kumbukumbu la Sheria 4:41-42 Biblia Habari Njema (BHN)
Ndipo Mose akatenga miji mitatu mashariki ya mto Yordani, ambamo mtu ataweza kukimbilia na kujisalimisha, kama ameua mtu ambaye si adui yake kwa bahati mbaya. Mtu kama huyo ataweza kukimbilia katika mji mmojawapo na kuyaokoa maisha yake.
Kumbukumbu la Sheria 4:41-42 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo Musa akabagua miji mitatu ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki; ili kwamba amwuaye mtu apate kukimbilia huko, amwuaye jirani yake pasipo kujua, wala hakumchukia tangu hapo; ili apate kuishi akimbiliapo mmojawapo miji hiyo
Kumbukumbu la Sheria 4:41-42 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo Musa akabagua miji mitatu ng’ambo ya Yordani upande wa matokeo ya jua; ili kwamba amwuaye mtu apate kukimbilia huko, amwuaye jirani yake pasipo kujua, wala hakumchukia tangu hapo; ili apate kuishi akimbiliapo mmojawapo miji hiyo
Kumbukumbu la Sheria 4:41-42 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kisha Musa akatenga miji mitatu mashariki mwa Yordani, ambayo mtu yeyote aliyemuua mtu angeweza kukimbilia ikiwa amemuua jirani yake bila kukusudia na bila kuwa na chuki naye siku zilizopita. Angeweza kukimbilia katika mmoja ya miji hii na kuokoa maisha yake.