Kumbukumbu la Sheria 4:27-28
Kumbukumbu la Sheria 4:27-28 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Mwenyezi Mungu atawatawanya miongoni mwa mataifa, na ni wachache wenu tu watakaosalia miongoni mwa mataifa hayo ambayo Mwenyezi Mungu atawafukuzia. Huko mtaabudu miungu ya miti na mawe iliyotengenezwa na watu, ambayo haiwezi kuona au kusikia wala kula au kunusa.
Kumbukumbu la Sheria 4:27-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu atawatawanya kati ya mataifa mengine, na ni wachache wenu tu watakaosalia huko ambako Mwenyezi-Mungu atawafukuzia. Huko mtaitumikia miungu ya miti na mawe ambayo imetengenezwa kwa mikono ya watu; na ambayo haiwezi kuona, haisikii, haili wala kunusa.
Kumbukumbu la Sheria 4:27-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na BWANA atawatawanya kati ya mataifa, nanyi mtasalia watu wachache kati ya makabila, mtakakopelekwa mbali na BWANA. Na huko mtatumikia miungu, waliotengenezwa kwa mikono ya watu, miti na mawe, miungu ambao hawaoni, hawasikii, hawali, wala hawanusi.
Kumbukumbu la Sheria 4:27-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na BWANA atawatawanya kati ya mataifa, nanyi mtasalia watu kidogo hesabu yenu kati ya makabila, mtakakopelekwa mbali na BWANA. Na huko mtatumikia miungu, kazi za mikono ya watu, miti na mawe, ambao hawaoni, wala hawasikii, hawali, wala hawanusi.