Kumbukumbu la Sheria 28:7-8
Kumbukumbu la Sheria 28:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Maadui zenu wakiwashambulia, Bwana atawapeni ushindi juu yao. Wakija kuwashambulia kwa njia moja watawakimbieni kwa njia saba. Baraka za Mwenyezi-Mungu zitakuwa katika ghala zenu za nafaka na katika shughuli zenu zote. Atawabariki katika nchi ambayo anawapeni.
Kumbukumbu la Sheria 28:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.
Kumbukumbu la Sheria 28:7-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.
Kumbukumbu la Sheria 28:7-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
BWANA atasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. BWANA ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako. BWANA Mungu wako atakubariki katika nchi anayokupa.