Kumbukumbu la Sheria 28:1-6
Kumbukumbu la Sheria 28:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
“Kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na kuzingatia kwa uangalifu amri ambazo ninawaamuru leo, yeye atawaweka juu ya mataifa yote duniani. Kama mkitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mtapewa baraka zifuatazo; “Miji yenu itabarikiwa na mashamba yenu. “Mtabarikiwa mpate wazawa wengi, mavuno mengi, ng'ombe na kondoo wengi. “Vikapu vyenu vya nafaka vitabarikiwa na vyombo vyenu vya kukandia. Mtabarikiwa mnaporudi nyumbani na mnapotoka nje.
Kumbukumbu la Sheria 28:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, kuongezeka kwa ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo wako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
Kumbukumbu la Sheria 28:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
Kumbukumbu la Sheria 28:1-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kama ukimtii BWANA Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii, BWANA Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia. Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama ukimtii BWANA Mungu wako: Utabarikiwa mjini na utabarikiwa mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na mazao ya nchi yako na wanyama wako wachanga wa kufugwa, yaani ndama wa makundi yako ya ngʼombe, na wana-kondoo wa makundi yako. Kapu lako na vyombo vyako vya kukandia vitabarikiwa. Utabarikiwa uingiapo na utabarikiwa utokapo.