2 Wakorintho 6:14-15
2 Wakorintho 6:14-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? Kuna mapatano gani kati ya Kristo na Beliari? Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini?
2 Wakorintho 6:14-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja? Kristo anawezaje kupatana na Shetani? Mwaamini ana uhusiano gani na asiyeamini?
2 Wakorintho 6:14-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
2 Wakorintho 6:14-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)