Yona 3:1-3 BHN
Neno la Mwenyezi-Mungu likamjia Yona mara ya pili: “Nenda Ninewi, ule mji mkuu, ukawatangazie watu ujumbe niliokupa.” Basi, Yona akaondoka, akaenda Ninewi kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza.
Mji wa Ninewi ulikuwa mkubwa sana. Upana wake ulikuwa mwendo wa siku tatu.