Yona 2:7-10 BHN
Roho yangu ilipoanza kunitoka,
nilikukumbuka, ee Mwenyezi-Mungu,
sala yangu ikakufikia,
katika hekalu lako takatifu.
Watu wanaoabudu sanamu za miungu batili,
huutupilia mbali uaminifu wao kwako.
Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,
nitakutolea sadaka,
na kutimiza nadhiri zangu.
Mwenyezi-Mungu, ndiye aokoaye.”
Basi, Mwenyezi-Mungu akamwamuru yule samaki, naye akamtapika Yona kwenye nchi kavu.