Yona 2:3-6 BHN
Ulinitupa katika kilindi, katikati ya bahari,
gharika ikanizunguka,
mawimbi na gharika vikapita juu yangu.
Nilidhani kwamba nimetengwa nisiwe mbele yako;
nisiweze kuliona tena hekalu lako takatifu.
Maji yalinizunguka na kunisonga;
kilindi kilinifikia kila upande,
majani ya baharini yakanifunika kichwa.
Niliteremka hadi kwenye misingi ya milima,
katika nchi ambayo milango yake imefungwa milele.
Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu,
umenipandisha hai kutoka humo shimoni.