Yeremia 5:29-31 BHN
“Je, nisiwaadhibu kwa mambo haya?
Je nitaacha kulipiza kisasi taifa kama hili?
Jambo la ajabu na la kuchukiza
limetokea katika nchi hii:
Manabii wanatabiri mambo ya uongo,
makuhani nao hutafuta faida yao wenyewe;
na watu wangu wanaona jambo hilo kuwa sawa. Lakini mwisho utakapofika mtafanyaje?”