Yeremia 5:27-28 BHN
Kama vile kapu lililojaa ndege walionaswa,
ndivyo nyumba zao zilivyojaa mali za udanganyifu.
Ndiyo maana wamekuwa watu wakubwa na matajiri,
wamenenepa na kunawiri.
Katika kutenda maovu hawana kikomo
hawahukumu yatima kwa haki wapate kufanikiwa,
wala hawatetei haki za watu maskini.