Yeremia 5:16-17 BHN
Mishale yao husambaza kifo;
wote ni mashujaa wa vita.
Watayala mazao yenu na chakula chenu;
watawamaliza watoto wenu wa kike na wa kiume.
Watachinja makundi yenu ya kondoo na ng'ombe;
wataiharibu mizabibu yenu na mitini yenu.
Miji yenu ya ngome mnayoitegemea,
wataiharibu kwa silaha zao.