Isaya 66:13-14 BHN
Kama mama amtulizavyo mwanawe,
kadhalika nami nitawatuliza;
mtatulizwa mjini Yerusalemu.
Mtayaona hayo na mioyo yenu itafurahi;
mifupa yenu itapata nguvu kama majani mabichi.
Hapo itajulikana kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huwalinda watumishi wangu,
lakini nikikasirika huwaadhibu maadui zangu.”