Mambo ya Walawi 7:22-24
Mambo ya Walawi 7:22-24 SRUV
BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Msile mafuta yoyote, ya ng'ombe, wala ya kondoo, wala ya mbuzi. Tena mafuta ya mnyama afaye mwenyewe, na mafuta ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, mna ruhusa kuyatumia kwa matumizi mengine; lakini msiyale kamwe.


