Kumbukumbu la Torati 4:25-26
Kumbukumbu la Torati 4:25-26 SRUV
Utakapozaa wana, na wana wa wana, mkisha kuwa katika nchi siku nyingi, mkajiharibu na kufanya sanamu ya kuchonga kwa umbo la kitu chochote, mkafanya ambayo ni maovu machoni pa BWANA Mungu wako, na kumtia hasira; naziita mbingu na nchi hivi leo kushuhudia, kwamba karibu mtaangamia kabisa juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki, hamtafanya siku zenu ziwe nyingi juu yake, ila mtaangamizwa kabisa.