Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 3

3
Nikodemo amtembelea Yesu
1 # Yn 7:50; 19:39 Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2#Mt 22:16 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, tunajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. 3#Mt 18:3; Lk 17:21; 1 Pet 1:23 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5#Eze 36:25-27; Efe 5:26; Tit 3:5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6#Yn 1:13; Mwa 5:3; Zab 51:5 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. 8#Mk 4:41; Mhu 11:5 Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho. 9Nikodemo akajibu, akamwambia, Mambo haya yawezaje kuwa? 10Yesu akajibu, akamwambia, Je! Wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu? 11#Yn 7:16; 8:26,28; 12:49 Amin, amin, nakuambia kwamba, Lile tulijualo tunalinena, na lile tuliloliona tunalishuhudia; wala ushuhuda wetu hamwukubali. 12#Lk 22:67 Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni? 13#Mit 30:4; Efe 4:9 Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu. 14#Hes 21:8,9 Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; 15ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
16 # Rum 5:8; 8:32; 1 Yoh 4:9 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17#Yn 5:22; 12:47; Lk 19:10; Mdo 17:31 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. 18#Yn 3:36; 5:24 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 19#Yn 1:5,9-11; 12:48 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. 20#Efe 5:13 Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. 21Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.
Yesu na Yohana Mbatizaji
22 # Yn 4:1,2 Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka katika nchi ya Yudea; akashinda huko pamoja nao, akabatiza. 23#Mt 4:12 Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa. 24#Mt 14:3; Mk 6:17; Lk 3:19-20 Maana Yohana alikuwa hajatiwa gerezani. 25Basi palitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja juu ya utakaso. 26#Yn 1:26-34 Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea. 27#Ebr 5:4 Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lolote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni. 28#Yn 1:20,23,27; Mk 1:2; Mt 11:10 Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nilisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. 29#Mt 9:15; 22:2 Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi. 30#2 Sam 3:1 Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.
Yeye atokaye mbinguni
31 # Yn 8:23 Yeye ajaye kutoka juu, huyo yuko juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yuko juu ya yote. 32#Yn 3:11 Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali ushuhuda wake. 33Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia mhuri ya kwamba Mungu ni kweli. 34#Yn 1:33,34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo. 35#Mt 11:27; Lk 10:22; Yn 5:20; 17:2 Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake. 36#Yn 3:18; Lk 3:7; 1 Yoh 5:12 Amwaminiye Mwana ana uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

Iliyochaguliwa sasa

Yohana 3: SRUVDC

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha