Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 14

14
Yesu ni njia ya kwenda kwa Baba
1 # Yn 14:27; Mk 11:22 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3#Yn 12:26; 17:24 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo. 4Nami niendako mwaijua njia. 5Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi tunaijuaje njia? 6#Ebr 10:20; Mt 11:27; Yn 11:25; Rum 5:1,2 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 7Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. 8Filipo akamwambia, Bwana, utuoneshe Baba, yatutosha. 9#Yn 12:45; Ebr 1:3; Mt 17:17 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuoneshe Baba? 10#Yn 12:49 Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. 11#Yn 14:20; Yn 10:25,38 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. 12#Mk 16:19,20 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. 13#Yn 15:7; Mk 11:24; 1 Yoh 5:14 Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14#Yn 16:23,24 Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya.
Ahadi ya kupewa Roho Mtakatifu
15 # Yn 15:10; 1 Yoh 5:3 Mkinipenda, mtazishika amri zangu. 16#Yn 14:26; 15:26; 16:7; 1 Yoh 2:1 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17#Yn 7:39; 16:13; Mt 10:20; Rum 8:26 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. 18Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. 19#Yn 16:16 Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. 20#Yn 17:21-23 Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu. 21#2 Kor 3:18; 1 Yoh 5:3 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. 22#Mdo 10:41 Yuda (siye Iskarioti), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? 23#Yn 13:34; 14:21; Mit 8:17; Mt 18:20; 28:20; Efe 3:17; 2 Kor 6:16 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. 24#Yn 7:16; 1 Yoh 2:5 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenituma.
25Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu. 26#Yn 14:16; Mt 10:19 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 27#Yn 1:16,33; Flp 4:7 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. 28#Yn 14:3,6,18; Lk 24:52 Mlisikia ya kwamba mimi niliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi. 29#Yn 13:19 Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, ili litakapotokea mpate kuamini. 30#Yn 12:31; Efe 2:2 Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana anakuja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. 31#Yn 10:18; Mt 26:46; Mk 14:42 Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.

Iliyochaguliwa sasa

Yohana 14: SRUVDC

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha