Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mt 16

16
Kudaiwa kwa Ishara
1 # Mk 8:11-21 # Mt 12:38; Lk 11:16 Wakamjia Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni. 2#Lk 12:54-56Akajibu, akawaambia, [Kukiwa jioni, mwasema, Kutakuwa na kianga; kwa maana mbingu ni nyekundu. 3#Mt 11:4Na asubuhi, mwasema, Leo kutakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa mbingu; lakini, je! Ishara za zamani hizi hamwezi kuzitambua?] 4#Mt 12:39; Lk 11:29; Yon 2:1Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake.
Chachu ya Mafarisayo na Masadukayo
5Nao wanafunzi wakaenda hata ng’ambo, wakasahau kuchukua mikate. 6#Lk 12:1Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo. 7Wakabishana wao kwa wao, wakisema, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate. 8#Mt 6:30Naye Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani chache, kwa sababu hamna mikate? 9#Mt 14:17-21Hamjafahamu bado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyoviokota? 10#Mt 15:34-38Wala ile mikate saba kwa watu elfu nne, na makanda mangapi mliyoyaokota? 11Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mkate naliwaambia? Ila jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo. 12#Yn 6:27Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.
Petro Amkiri Yesu kuwa Kristo
13 # Mk 8:27-30; Lk 9:18-21 Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? 14#Mt 14:1-2; 17:10; Mk 6:14-15; Lk 9:7-8Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. 15Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16#Yn 6:68-69Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. 17#Gal 1:15,16; Mt 17:4,5Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18#Yn 1:42; Efe 2:20Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
19 # Mt 18:18; Yn 20:23 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. 20#Mt 17:9Ndipo alipowakataza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ye yote ya kwamba yeye ndiye Kristo.
Yesu Asema juu ya Kufa na Kufufuka kwake
21 # Mk 8:31—9:1; Lk 9:22-27 # Mt 12:40; Yn 2:19 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. 22Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. 23Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
Msalaba na Kujikana
24 # Mt 10:38; Lk 14:27 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. 25#Mt 10:39; Lk 17:33; Yn 12:25Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. 26#Mt 4:8Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 27#Mt 25:31; Zab 62:12; Rum 2:6; Yn 5:29; Mit 24:12Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 28#Mt 10:23Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.

Iliyochaguliwa sasa

Mt 16: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha