Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mt 14

14
Kuuawa kwa Yohana Mbatizaji
1 # Mk 6:14,17-30; Lk 9:7-9 # Lk 3:19,20 Wakati ule mfalme Herode alisikia habari za Yesu, akawaambia watumishi wake, 2Huyo ndiye Yohana Mbatizaji; amefufuka katika wafu; na kwa hiyo nguvu hizo zinatenda kazi ndani yake. 3#Lk 3:19-20; Mt 11:2Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodia, mke wa Filipo nduguye. 4#Law 18:16; 20:21Kwa sababu Yohana alimwambia, Si halali kwako kuwa naye. 5#Mt 21:26Naye alipotaka kumwua, aliwaogopa watu, maana walimwona Yohana kuwa nabii. 6Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode. 7Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lo lote atakaloliomba. 8Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. 9Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe; 10#Mt 17:12akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani. 11Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana; akakichukua kwa mamaye. 12Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.
Kulishwa kwa Watu Elfu Tano
13 # Mk 6:31-44; Lk 9:10-17; Yn 6:1-13 Naye Yesu aliposikia; hayo, aliondoka huko katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa miguu kutoka mijini mwao. 14#Mt 9:36Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao. 15Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula. 16Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi vyakula. 17Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili. 18Akasema, Nileteeni hapa. 19Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano. 20#2 Fal 4:44Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa. 21Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.
Yesu Atembea juu ya Maji
22 # Mk 6:45-56; Yn 6:15-21 Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng’ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano. 23#Lk 6:12; 9:18Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake. 24Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho. 25Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. 26#Lk 24:37Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu. 27Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope. 28Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. 29Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. 30Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. 31#Mt 8:26Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? 32Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma. 33Nao waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu.
Yesu Awaponya Wagonjwa katika Genesareti
34Na walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti. 35Na watu wa mahali pale walipomtambua, walituma watu kwenda nchi zile zilizo kandokando, wakamletea wote waliokuwa hawawezi; 36#Mt 9:21; Lk 6:19nao wakamsihi waguse hata pindo la vazi lake tu; na wote waliogusa wakaponywa kabisa.

Iliyochaguliwa sasa

Mt 14: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha