Zaburi 119:5-8
Zaburi 119:5-8 NEN
Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara katika kuyatii maagizo yako! Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia amri zako zote. Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki. Nitayatii maagizo yako; usiniache kabisa.




