Zaburi 110
110
Zaburi 110
Bwana na mfalme wake mteule
Zaburi ya Daudi.
1 Bwana amwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
hadi nitakapowafanya adui zako
kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
2 Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;
utatawala katikati ya adui zako.
3 Askari wako watajitolea kwa hiari
katika siku yako ya vita.
Ukiwa umevikwa fahari takatifu,
kutoka tumbo la mapambazuko
utapokea umande wa ujana wako#110:3 au vijana wako watakujia kama umande.
4 Bwana ameapa,
naye hatabadilisha mawazo yake:
“Wewe ni kuhani milele,
kwa mfano wa Melkizedeki.”
5 Bwana yuko mkono wako wa kuume,
atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.
6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga
na kuwaponda watawala wa dunia nzima.
7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia#110:7 au Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka;;
kwa hiyo atainua kichwa chake juu.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 110: NEN
Kuonyesha
Nakili
Linganisha
Shirikisha
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Holy Bible, Kiswahili Contemporary Version™ (Neno: Biblia Takatifu™) | Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. | Used with permission. All rights reserved worldwide.
Biblica® Cross Reference System | Copyright © 2025 by Biblica, Inc. | Used with permission. All rights reserved worldwide.