Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 32:14-15

Yeremia 32:14-15 NENO

‘Hili ndilo asemalo BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli: Chukua hati hizi, yaani nakala zote zenye muhuri na zisizo na muhuri za hati ya kununulia, na uziweke kwenye gudulia la udongo wa mfinyanzi ili zidumu kwa muda mrefu. Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli: Nyumba, mashamba na mashamba ya mizabibu yatanunuliwa tena katika nchi hii.’