Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waamuzi 2:8-10

Waamuzi 2:8-10 NENO

Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa BWANA, akafa akiwa na umri wa miaka mia moja na kumi. Wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-Heresi katika nchi ya vilima ya Efraimu, kaskazini mwa Mlima Gaashi. Baada ya kizazi kile chote kukusanywa pamoja na baba zao, kikainuka kizazi kingine baada yao ambacho hakikumjua BWANA, wala matendo yale aliyokuwa ametenda kwa ajili ya Waisraeli.