1
Isa 54:17
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
SUV
Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.
Linganisha
Chunguza Isa 54:17
2
Isa 54:10
Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye.
Chunguza Isa 54:10
3
Isa 54:4
Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena.
Chunguza Isa 54:4
4
Isa 54:5
Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.
Chunguza Isa 54:5
5
Isa 54:2
Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako.
Chunguza Isa 54:2
6
Isa 54:13
Na watoto wako wote watafundishwa na BWANA; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.
Chunguza Isa 54:13
7
Isa 54:8
Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema BWANA, Mkombozi wako.
Chunguza Isa 54:8
8
Isa 54:7
Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya.
Chunguza Isa 54:7
9
Isa 54:9
Kwa maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama nilivyoapa ya kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba sitakuonea hasira, wala kukukemea.
Chunguza Isa 54:9
10
Isa 54:12
Nami nitaifanya minara yako ya akiki nyekundu, na malango yako ya almasi, na mipaka yako yote ya mawe yapendezayo.
Chunguza Isa 54:12