YouVersion Logo
Search Icon

Njia Ya Mungu Ya MafanikioSample

Njia Ya Mungu Ya Mafanikio

DAY 3 OF 3

Hakuna mtu anayepanga kushindwa. Na ingawa hatuwezi kurudi nyuma na kutengua makosa ya miaka yetu ya zamani, tuna chaguo la kufanikiwa kutoka hapa na kuendelea. Tunaweza kuanza au kuendelea na safari ya kutimiza majaliwa ya Mungu kwetu.

Mungu anatupa siri ya kuishi maisha ya mafanikio katika Zaburi 25:14. Kujua agano la Mungu ni kujua kibali chake na baraka zake. Agano lake linafungamana wazi wazi na kifuniko chake. Jifungamanishe chini ya utawala wa kanuni ya agano ya Mungu maishani na utapata mafanikio ya kiroho.

Lakini aya hii ina sharti: unapata tu kujua agano la Mungu kwa kumcha. Kuna hali ya sababisho na athari ya mazingira ili kuyapata mafanikio ya kiroho. Ni kuhusu kile unachofanya kuhusiana na heshima na adhama unayoonyesha kwa Mungu na neno lake. Hii itaathiri moja kwa moja kiwango chako cha mafanikio ya kiroho. Huwezi kumvunjia Mungu heshima katika maamuzi yako ukategemea kufikia kiwango chochote cha mafanikio ya ufalme. Mafanikio huanza kwa heshima na utii.

Ni sehemu gani za maisha yako ambapo hauonyeshi kicho ifaayo kwa Mungu?

Je, inamaanisha nini kuwa na agano na Mungu?

Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.

Day 2

About this Plan

Njia Ya Mungu Ya Mafanikio

Kila mtu anatafuta mafanikio, lakini wengi hawayapati kwa sababu wanachofuata ni ufahamu potofu wa nini maana ya kuishi maisha ya mafanikio. Ili kupata mafanikio ya kweli unahitaji kuweka macho yako katika ufafanuzi wa Mungu wa maana yake. Mruhusu mwandishi wa vitabu vinavyouzwa sana Tony Evans akuonyeshe njia ya mafanikio ya kweli ya ufalme na jinsi unavyoweza kuipata.

More