YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 09/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

DAY 20 OF 30

Mungu aliamuru Ezekieli kuwajulisha Yerusalemu juu ya uovu wao kuwa ni pamoja na uonevu uliomwaga damu za wanyonge, uongo, ukatili, ibada za sanamu na tamaa za mwili (m.6-12). Ndipo Mungu anatangaza adhabu au hukumu kwao (m.13-16). Ni vizuri kujadiliana na kuona kama uovu uliotendwa na Yerusalemu upo hata kwetu leo. Linganisha na yale tunayoyasikia kwenye vyombo vya habari leo; ubakaji, wizi, uuaji kwa imani za kishirikina, haya yote yatufanye kuona haja ya kuingia kwenye toba ya kweli.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More