YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 09/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

DAY 18 OF 30

Ezekieli anaelezea kuwa Mungu atakapoamua kuadhibu waliomwasi, hakuna atakayeweza kuiepuka ghadhabu hiyo (m.47-48, Tazama nitawasha moto ndani yako, nao utakula kila mti mbichi ndani yako, na kila mti mkavu; miali ya moto ule haitazimika, na nyuso zote toka kusini hata kaskazini zitateketezwa kwa moto huo.  Na watu wote wenye mwili wataona ya kuwa mimi, Bwana, nimeuwasha; hautazimika). Ikumbukwe kuwa siku zote BWANA MUNGU anachukia uovu, na kila tutendapo uovu tunasababisha ghadhabu yake kuwaka juu yetu. Hata hivyo yeye ni mwingi wa rehema, anatualika kutubu.Ugua, basi, Ee mwanadamu; kwa kuvunjika kwake viuno vyako, na kwa uchungu, utaugua mbele ya macho yao(m.6). Hivyo msomaji wa somo hili leo, usifanye moyo wako kuwa mgumu. Jitafakari juu ya mahusiano yako na Mungu, kisha tafuta kutubu na kuanza maisha mapya yapatanayo na toba.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More