YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 09/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

DAY 16 OF 30

Waisraeli waliishi katika mapokea ya baba zao ambayo yalikuwa kinyume na Neno la Mungu. Msiende katika amri za baba zenu, wala msizishike hukumu zao, wala msijitie unajisi kwa vinyago vyao(m.18). Watoto hao waliniasi; hawakuenda katika amri zangu (m.21). Kwa sababu hawakuzitekeleza hukumu zangu, bali walizikataa amri zangu, nao walizitia unajisi sabato zangu, na macho yao yaliandama vinyago vya baba zao (m.24). Hata siku hizi kuna madhehebu na huduma nyingi zinazohubiri na kufundisha neno la Mungu. Baadhi ya mafundisho yanatofautiana sana na Biblia. Kifungu hiki kinatufundisha kuwa Neno la Mungu lililo sahihi na lisilobadilika ni Biblia. Hivyo kila Mkristo awe na Biblia, na tujenge mazoea ya kujisomea na kutafakari yaliyomo ndani yake. Kisha tumruhusu Roho wa Mungu kusema nasi katika roho.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More