YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 09/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

DAY 12 OF 30

Israeli walimlalamikia Mungu kuwa anawaadhibu kwa dhambi ambazo walizifanya baba zao. Ndipo Mungu kupitia nabii Ezekieli anawakumbusha kuwa Mungu ni mwaminifu ambaye hawezi kumwadhibu mtu kwa sababu ya mtu mwingine, ila kila mtu anadhibiwa kutokana na uovu wake. Linapotokea jambo baya, mara nyingi watu hupenda kuwasingizia wengine ili wao waonekane kuwa safi. Kumbe neno hili linatutaka kila mmoja kujichunguza na kutubu dhambi yake binafsi kabla ya kuwatazama wengine.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More