YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 09/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

DAY 10 OF 30

Nabii Ezekieli anatumia mfano wa tai, tawi la mti (m.1-4) na tawi la mzabibu (m.7-8), kwa lengo la kufafanua dhambi ya udanganyifu aliyoifanya Sedekia dhidi ya Babeli (2 Fal 24:20, Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli). Ni kitendo cha kuwategemea wanadamu badala ya kumtegemea Mungu katika vita. Hii ni dhambi ambayo baadhi ya wanadamu huitenda. Unapomwamini mtu kuliko Mungu ni kumkosea Mungu. Tunapowapenda watu zaidi kuliko kumpenda Mungu, pia tunakuwa tunamkosea Mungu. Siku zote Mungu awe namba moja.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More