YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Soma Biblia Kila Siku 10

DAY 5 OF 31

Katika m.20 Paulo ameeleza kuwa mtu akikutana na sheria ya Mungu anatambua zaidi dhambi zake na upotevu wake, kwa hiyo hata neema ya Mungu kwake inaonekana kubwa zaidi: "Kumbe! Neema ya Mungu ni kubwa namna hii kwamba hata mimi nimeweza kusamehewa na kuwa mtoto wake!" Ndipo Paulo anauliza swali ambalo limesikika hata Tanzania: Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? (m.1). Jibu lake ni kuwa sisi tuliouona ubaya wa dhambi na kuupokea ukombozi kwa damu ya Yesu tutaendeleaje kuipenda dhambi? (m.2: Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?).