Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Mungu alijua kwamba sisi wanadamu hatuwezi wenyewe kusafisha maisha yetu. Hatuna haki wala utakatifu unaotustahilisha kuingia Mbinguni na kusimama mbele ya Mungu Mtakatifu! Aliona tumepotea. Ndipo akaamua kwa upendo wake kufanya upatanisho kwa njia ya Mwana wake Yesu Kristo ili tusafishwe katika damu yake. Kazi hii ya wokovu ni kazi aliyoifanya Mungu peke yake. Hapakuwa na ustahili wowote kwetu uliomfanya atende hivyo. Sababu ni moja tu: upendo wake! Zingatia m.8-10:Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Fungua moyo wako leo, umpokee Yesu!
Scripture
About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Warumi na 1 Samweli.
More
Related Plans

Finding Joy

Elijah: A Man Surrendered to God

And He Dwelt

The Layoff Test: Trusting God Through a Season of Unemployment

The Power of Biblical Meditation

Joyfully Expecting!

Between the Altar and the Father’s Embrace

Mom in the Word: One-Year Bible Plan (Volume 1)

God’s Word, Her Mission: Encouragement for Women Helping Build God’s Kingdom by Wycliffe Bible Translators
