YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10Sample

Soma Biblia Kila Siku 10

DAY 2 OF 31

Maana ya mstari wa kwanza unaonekana vizuri zaidi katika Kiswahili cha kisasa (Habari Njema): Sasa, kwa vile tumefanywa kuwa waadilifu kwa imani, basi tunayoamani naye Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.Ndugu msomaji, naomba habari hii njema uipokee ipate kukufariji! Kushinda kwako katika hukumu ya Mungu siku ya mwisho kunategemea Yesu Kristo peke yakewala hakutegemei tendo lo lote kwako. Huna sababu ya kuhofu unapomwamini Yesu, maana amani na Mungu umepata bure kwa neema kwa njia ya Yesu Kristo! Zingatia m.2 na m.9-10: Kwa yeye [Yesu Kristo] tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. ...Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.

Scripture