YouVersion လိုဂို
ရွာရန္ အိုင္ကြန္

Somabiblia Kila Siku 3နမူနာ

Somabiblia Kila Siku 3

31 ၏ ေန႔ 1

Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa (m.21 na 32). Kwa macho ya kibinadamu Bwana Yesu alichelewa. Lakini Yesu alijua yote tokea mbali (m.11-15). Na ilikuwa ni hatari kwa Yesu kwenda Bethania (m.7-8 na 16). Lakini upendo wake kwa wafiwa ulimsukuma aende (m.3 na 5)! Martha alipoonyesha imani yake juu ya ufufuo siku ya mwisho (m. 23f), Yesu alimfundisha akisema: Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi(m.25f)! Je, unasadiki hayo?