Logo YouVersion
Icona Cerca

Mwanzo 1

1
Siku sita za uumbaji na Sabato
1 # Yn 1:1,3; Ebr 1:10; Ayu 38:4; Isa 44:24; Rum 1:20; Kol 1:16; Ebr 11:3; Ufu 4:11 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2#Yer 4:23; Isa 40:12 Nayo nchi ilikuwa tupu, tena bila umbo, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3#2 Kor 4:6; Zab 33:9 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. 5#Zab 74:16 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
6 # Ayu 37:18; Zab 33:6; 136:5; Yer 10:12; 2 Pet 3:5 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. 7Mungu akaliumba anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. 8Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.
9 # Ayu 26:10; 38:8; Zab 33:7; 95:5 Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. 10Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 11#Ebr 6:7; Lk 6:44 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mimea itoayo mbegu, na miti ya matunda izaayo matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. 12Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 13Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.
14 # Kum 4:19; Ayu 25:3,5; Zab 74:16; 136:7 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili ya kuonesha majira, siku na miaka; 15tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. 16Mungu akaumba mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. 17#Zab 8:1 Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi 18na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 19Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.
20 # Zab 104:24 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na viumbe vyenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. 21Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 22Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi. 23Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.
24 # Zab 104:18-23 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. 25Mungu akaumba aina zote za wanyama wa porini na wa kufugwa na viumbe vyote vitambaavyo nchini; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 26#Zab 100:3; Efe 4:24; Yak 3:9; Zab 8:6 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila kiumbe kitambaacho nchini. 27#1 Kor 11:7; Efe 4:24; Kol 3:10; Mal 2:15; Mt 19:4; Mk 10:6; Mwa 5:1-2 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28#Zab 127:3; 1 Tim 4:3; Mwa 9:1,7; Law 26:9; Zab 128:3,4 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. 29#Ayu 36:31; Zab 104:14,15; 136:25; 146:7; Mdo 14:17 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mmea utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa chakula chenu; 30#Zab 145:15,16; 147:9; Ayu 38:41 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. 31#Zab 104:24; 1 Tim 4:4 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.

Attualmente Selezionati:

Mwanzo 1: SRUVDC

Evidenziazioni

Condividi

Copia

None

Vuoi avere le tue evidenziazioni salvate su tutti i tuoi dispositivi?Iscriviti o accedi

YouVersion utilizza i cookie per personalizzare la tua esperienza. Utilizzando il nostro sito Web, accetti il nostro utilizzo dei cookie come descritto nella nostra Privacy Policy