YouVersion Logo
Search Icon

Methali 22

22
1Afadhali kuwa na sifa nzuri kuliko mali nyingi;
wema ni bora kuliko fedha au dhahabu.
2Matajiri na maskini wana hali hii moja:
Mwenyezi-Mungu ni Muumba wao wote.
3Mtu mwangalifu huona hatari akajificha,
lakini wajinga hujitokeza mbele wakaumia.
4Ukinyenyekea na kumcha Mwenyezi-Mungu,
utapata tuzo: Fanaka, heshima na uhai.
5Njia ya waovu imejaa miiba na mitego;
anayetaka kuhifadhi maisha yake ataiepa.
6Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri,
naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni.
7Tajiri humtawala maskini;
mkopaji ni mtumwa wa mkopeshaji.
8Apandaye dhuluma atavuna janga;
uwezo wake wa kutenda mabaya utavunjwa.
9Mtu mkarimu atabarikiwa,
maana chakula chake humgawia maskini.
10Mfukuze mwenye dharau na fujo itatoweka,
ugomvi na matusi vitakoma.
11Mwenye nia safi na maneno mazuri,
atakuwa rafiki wa mfalme.
12Mwenyezi-Mungu hulinda elimu ya kweli,
lakini huyavuruga maneno ya waovu.
13Mvivu husema, “Siwezi kutoka nje;
kuna simba huko, ataniua!”
14Kinywa cha mwasherati ni shimo refu;
anayechukiwa na Mwenyezi-Mungu atatumbukia humo.
15Mtoto hupenda mambo ya kijinga moyoni,
lakini fimbo ya nidhamu humwondolea hayo.
16Anayemdhulumu maskini atamfanya afaidike mwishowe,
anayewapa matajiri zawadi ataishia kuwa maskini.
Misemo thelathini ya wenye hekima
17Tega sikio usikie maneno ya wenye hekima,
elekeza moyo wako uzingatie maarifa yangu.
18Wewe utafurahi endapo utayaweka moyoni,
na kuyakariri kila wakati.
19Ninayependa kumfundisha leo ni wewe,
ili tegemeo lako liwe kwa Mwenyezi-Mungu.
20Nimekuandikia misemo thelathini,
misemo ya maonyo na maarifa,
21ili kukufundisha yaliyo sawa na kweli;
na mtu akikuuliza uweze kumpa jibu sahihi.
- 1 -
22Usimdhulumu maskini kwa kuwa ni maskini,
wala usimnyime fukara haki yake mahakamani.
23Maana Mwenyezi-Mungu atawatetea;
atawapokonya maisha yao wale watakaowadhulumu.
- 2 -
24Usifanye urafiki na mtu wa hasira,
wala usiandamane na mwenye ghadhabu,
25usije ukajifunza mwenendo wake,
ukajinasa kabisa katika mtego.
- 3 -
26Usiwe mmoja wao wenye kuweka ahadi,
watu ambao hujiweka wadhamini wa madeni.
27Ikiwa huna chochote cha kulipa,
hata kitanda unacholalia kitachukuliwa!
- 4 -
28Usiondoe alama ya mipaka ya zamani
ambayo iliwekwa na wazee wako.
- 5 -
29Je, yuko mtu mwenye maarifa kazini mwake?
Huyo atawatumikia wafalme;
hatawapa huduma yake watu wasiofaa.
- 6 -

Currently Selected:

Methali 22: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy