YouVersion Logo
Search Icon

Mit 1

1
KITABU CHA KWANZA
1 # 1 Fal 4:32 Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.
Utangulizi
2Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; 3#Mit 2:1kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. 4Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na hadhari; 5mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia. 6Kufahamu mithali na kitendawili, na maneno ya wenye hekima na mafumbo yao. 7#Ayu 28:28; Zab 111:10; Mit 9:10Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Maonyo dhidi ya Kushirikiana na Waovu
8Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako,
Wala usiiache sheria ya mama yako,
9Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako,
Na mikufu shingoni mwako.
10 # Mwa 39:7; Amu 16:16-21; Rum 16:18; Efe 5:11 Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi,
Wewe usikubali.
11 # Mit 12:6; Yer 5:26; Mik 7:2 Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi,
Na tuvizie ili kumwaga damu;
Tumwotee asiye na hatia, bila sababu;
12 # Zab 28:1 Tuwameze hai kama kuzimu,
Na wazima, kama wao washukao shimoni.
13Tutapata mali yote ya thamani,
Tutazijaza nyumba zetu mateka.
14Wewe utashirikiana nasi;
Tutakuwa na vitu vyote shirika.
15 # Mit 4:14 Mwanangu, usiende njiani pamoja nao;
Uzuie mguu wako usiende katika mapito yao.
16 # Isa 59:7 Maana miguu yao huenda mbio maovuni,
Nao hufanya haraka ili kumwaga damu.
17Kwa kuwa mtego hutegwa bure,
Mbele ya macho ya ndege ye yote.
18Na hao hujiotea damu yao wenyewe,
Hujinyemelea nafsi zao wenyewe.
19 # 2 Fal 5:20-27; Mik 2:1-3; 1 Tim 6:10 Ndivyo zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali;
Huuondoa uhai wao walio nayo.
Wito wa Hekima
20 # Mit 8:1-3 Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu,
Hutoa sauti yake katika viwanja;
21Hulia penye mikutano mikubwa ya watu,
Mahali pa kuyaingilia malango,
Ndani ya mji hutamka maneno yake.
22Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga?
Na wenye dharau kupenda dharau yao,
Na wapumbavu kuchukia maarifa?
23 # Yoe 2:28; Yn 7:37 Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu;
Tazama, nitawamwagia roho yangu,
Na kuwajulisheni maneno yangu.
24 # Isa 66:4; Yer 7:13; Zek 7:11 Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa;
Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu;
25 # Lk 7:30 Bali mmebatilisha shauri langu,
Wala hamkutaka maonyo yangu;
26Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu,
Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;
27Hofu yenu ifikapo kama tufani,
Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli,
Dhiki na taabu zitakapowafikia.
28 # Isa 1:15; Yer 14:12; Mik 3:4; Yak 4:3 Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika;
Watanitafuta kwa bidii, wasinione.
29 # Ayu 21:14; Zab 50:16,17; Isa 27:11; Yn 3:20; Mdo 7:51 Kwa kuwa walichukia maarifa,
Wala hawakuchagua kumcha BWANA.
30Hawakukubali mashauri yangu,
Wakayadharau maonyo yangu yote.
31 # Isa 3:11 Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao,
Watashiba mashauri yao wenyewe.
32Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua,
Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.
33Bali kila anisikilizaye atakaa salama,
Naye atatulia bila kuogopa mabaya.

Currently Selected:

Mit 1: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy