YouVersion Logo
Search Icon

Yn 4

4
Yesu na Mwanamke Msamaria
1 # Yn 3:22,26 Kwa hiyo Bwana, alipofahamu ya kuwa Mafarisayo wamesikia ya kwamba, Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kuwabatiza, 2#1 Kor 1:17(lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake,) 3aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya. 4#Lk 9:52Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria. 5#Mwa 33:19; 48:22; Yos 24:32Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe. 6Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita. 7Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe. 8Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula. 9#Ezr 4:1-5; Neh 4:1-2; Lk 9:53Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.) 10#Yn 7:38,39Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai. 11Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai? 12#Yn 8:53Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake? 13#Yn 6:58Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; 14#Yn 6:27,35; Yn 7:37-39walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. 15Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka. 16Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. 17Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume; 18kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli. 19#1 Kor 14:24,25; Yn 9:17Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! 20#Kum 12:5; Zab 122:1-9Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. 21#Mk 14:58Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. 22#2 Fal 17:29-41; Isa 2:3Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. 23Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 24#Rum 12:1; 2 Kor 3:17Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. 25#Yn 1:41Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote. 26#Yn 9:37; 10:25Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye.
27Mara hiyo wakaja wanafunzi wake, wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hakuna aliyesema, Unatafuta nini? Au, Mbona unasema naye? 28Basi yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu, 29Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo? 30Basi wakatoka mjini, wakamwendea. 31Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabi, ule. 32#Yn 4:34Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi. 33Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula? 34#Yn 17:4Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake. 35#Mt 9:37; Lk 10:2Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno. 36Naye avunaye hupokea mshahara, na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wapate kufurahi pamoja. 37#Mik 6:15Kwa maana hapo neno hilo huwa kweli, Mmoja hupanda akavuna mwingine. 38Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao.
39Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda. 40Basi wale Wasamaria walipomwendea, walimsihi akae kwao; naye akakaa huko siku mbili. 41Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya neno lake. 42#1 Yoh 4:14Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu.
Yesu Arudi Galilaya
43 # Mt 4:12 Na baada ya siku mbili hizo akaondoka huko, akaenda Galilaya. 44#Mt 13:57; Mk 6:4; Lk 4:24Kwa maana Yesu mwenyewe alishuhudia ya kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe. 45#Yn 2:23Basi alipotoka Galilaya, Wagalilaya walimpokea; kwa kuwa wameyaona mambo yote aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu; maana hao nao waliiendea sikukuu.
Yesu Amponya Mwana wa Ofisa
46 # Yn 2:1-11 Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu. 47#Lk 7:2Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa kufani. 48#Yn 2:18; 1 Kor 1:22Basi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa? 49Yule diwani akamwambia, Bwana, ushuke asijakufa mtoto wangu. 50Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia. 51#Mt 8:6Hata alipokuwa akishuka, watumwa wake walimlaki, wakisema ya kwamba mtoto wake yu hai. 52Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa hajambo; nao wakamwambia, Jana, saa saba, homa ilimwacha. 53#Lk 19:9; Mdo 16:15,31Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake. 54#Yn 2:11,23Hiyo ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu, alipokuwa ametoka Uyahudi kufika Galilaya.

Currently Selected:

Yn 4: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy