YouVersion Logo
Search Icon

Yn 14

14
Yesu ni Njia ya kwenda kwa Baba
1 # Yn 14:27; Mk 11:22 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3#Yn 12:26; 17:24Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. 4Nami niendako mwaijua njia. 5Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? 6#Ebr 10:20; Mt 11:27; Yn 11:25; Rum 5:1,2Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 7Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. 8Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. 9#Yn 12:45; Ebr 1:3; Mt 17:17Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? 10#Yn 12:49Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. 11#Yn 14:20; Yn 10:25,38Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. 12#Mk 16:19,20Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. 13#Yn 15:7; Mk 11:24; 1 Yoh 5:14Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14#Yn 16:23,24Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.
Ahadi ya kupewa Roho Mtakatifu
15 # Yn 15:10; 1 Yoh 5:3 Mkinipenda, mtazishika amri zangu. 16#Yn 14:26; 15:26; 16:7; 1 Yoh 2:1Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17#Yn 7:39; 16:13; Mt 10:20; Rum 8:26ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. 18Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. 19#Yn 16:16Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. 20#Yn 17:21-23Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu. 21#2 Kor 3:18; 1 Yoh 5:3Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. 22#Mdo 10:41Yuda (siye Iskariote), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? 23#Yn 13:34; 14:21; Mit 8:17; Mt 18:20; 28:20; Efe 3:17; 2 Kor 6:16Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. 24#Yn 7:16; 1 Yoh 2:5Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.
25Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu. 26#Yn 14:16; Mt 10:19Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 27#Yn 1:16,33; Flp 4:7Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. 28#Yn 14:3,6,18; Lk 24:52Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi. 29#Yn 13:19Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, kusudi litakapotokea mpate kuamini. 30#Yn 12:31; Efe 2:2Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. 31#Yn 10:18; Mt 26:46; Mk 14:42Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.

Currently Selected:

Yn 14: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy