YouVersion Logo
Search Icon

Yak 1

1
Salamu
1 # Mt 13:55; Mk 6:3; Mdo 15:13,23; 1 Pet 1:1; Gal 1:19 Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika; salamu.
Imani na Hekima
2 # Rum 5:3-5; 1 Pet 1:6 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3#1 Pet 1:7mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. 4Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
5 # Mit 2:3-6 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. 6#Mk 11:24Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. 7Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. 8Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.
Umaskini na Utajiri
9 # Yak 2:5 Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa; 10#Isa 40:6-7; 1 Pet 1:24bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka. 11Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.
Majaribu na Mateso
12 # Dan 12:12; 2 Tim 4:8; 1 Pet 5:4; 1 Kor 9:25; Ufu 2:10 Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. 13Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. 14#Rum 7:7-10Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. 15Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. 16Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike. 17#1 Yoh 1:5; Mt 7:11Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. 18#Yn 1:13; 1 Pet 1:23Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.
Kusikia na Kutenda Neno
19 # Mhu 7:9 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika; 20#Efe 4:26kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu. 21#Kol 3:8; 1 Pet 2:1Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. 22#Mt 7:26; Rum 2:13Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. 23Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. 24Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. 25#Yak 2:12; Rum 8:2; Yn 13:17Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake. 26#Zab 34:13Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. 27Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

Currently Selected:

Yak 1: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy