YouVersion Logo
Search Icon

Mhu 1

1
Ubatili wa Maisha
1Maneno ya Mhubiri#1:1 Kiebrania ni Koheleth, yaani, Mhubiri, au Mshauri., mwana wa Daudi, mfalme katika Yerusalemu 2#Zab 39:5; 62:9,10; Mhu 4:4-6; Rum 8:20Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili. 3#Mhu 3:9Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?
4 # Zab 104:5; 2 Pet 3:10 Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. 5#Zab 19:5Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake. 6#Yn 3:8Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake. 7#Ayu 38:10; Zab 104:8Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.
8 # Mhu 3:1; Mit 27:20 Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.
9 # Mwa 8:22; Mhu 3:15 Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua. 10Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi.
11Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye.
Ubatili wa Kutafuta Hekima
12Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu. 13#Mwa 3:19; Mhu 3:10Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. 14Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo.
15 # Mhu 7:13 Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa,
Wala yasiyokuwapo hayahesabiki.
16 # 1 Fal 4:29-31; 3:12; Mhu 2:9 Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa. 17#Mhu 2:3; 1 The 5:21Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kujilisha upepo. 18#Ayu 28:28; Mhu 7:16; 1 Kor 1:20Yaani,
Katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni;
Naye aongezaye maarifa huongeza masikitiko.

Currently Selected:

Mhu 1: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy