YouVersion Logo
Search Icon

1 Nya 1

1
Toka Adamu hadi Abrahamu
1 # Mwa 4:25; 5:3,9 Adamu, na Sethi, na Enoshi; 2na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi; 3#Yud 1:14na Henoko, na Methusela, na Lameki; 4na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi.
5 # Mwa 10:2 Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. 6Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. 7Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani.
8 # Mwa 16:0 Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. 9Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani. 10#Mwa 10:8,13Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. 11Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, 12#Mwa 10:14; Kum 2:23; Yer 47:4; Amo 9:7na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori. 13Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi; 14na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi; 15na Mhivi, na Mwarki, na Msini; 16na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi.
17 # Mwa 9:23,26; 10:22; 11:10 Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. 18Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi. 19Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani. 20Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera; 21na Hadoramu, na Uzali, na Dikla; 22na Obali, na Abimaeli, na Sheba; 23na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
24 # Mwa 11:10; Lk 3:36 Shemu, na Arfaksadi, na Sala; 25#Mwa 11:15; Hes 24:24; Lk 3:35na Eberi, na Pelegi, na Reu; 26na Serugi, na Nahori, na Tera; 27#Mwa 17:5; 2 Nya 20:7; Neh 9:7; Isa 41:8; 51:2; Rum 4:16; Yak 2:23na Abramu, naye ndiye Ibrahimu.
Toka Abrahamu hadi Yakobo
28 # Mwa 21:2,3; 16:11,15 Wana wa Ibrahimu; Isaka, na Ishmaeli.
29 # Mwa 25:13-16 Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu; 30#Mwa 25:15na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema; 31na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
32 # Mwa 25:1,2 Na wana wa Ketura, suria yake Ibrahimu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani. 33Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura.
34 # Mwa 21:2,3; 25:25 Na Ibrahimu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli.
35 # Mwa 36:9,10; Kum 2:22; Mal 1:2,3; Rum 9:13; Ebr 12:16 Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora. 36#Mwa 36:11Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki. 37Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza. 38#Mwa 36:20Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani. 39#Mwa 36:22Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni umbu lake Lotani. 40#Mwa 36:23Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana. 41#Mwa 36:25,26Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. 42#Mwa 36:27Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani.
43 # Mwa 36:31; 49:10 Basi hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla hajamiliki mfalme awaye yote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba. 44Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akamiliki badala yake. 45Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akamiliki badala yake. 46#1 Fal 11:14Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akamiliki badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi. 47Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akamiliki badala yake. 48#Mwa 36:37Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akamiliki badala yake. 49Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akamiliki badala yake. 50#Mwa 36:39Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akamiliki badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. 51#Mwa 36:40; Kut 15:15Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi; 52na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni; 53na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari; 54na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.

Currently Selected:

1 Nya 1: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy