Zaburi 134:1-3

BHN
Biblia Habari Njema

1Njoni kumsifu Mwenyezi-Mungu enyi watumishi wake wote,
enyi nyote mnaotumikia usiku nyumbani mwake.
2Inueni mikono kuelekea mahali patakatifu,
na kumtukuza Mwenyezi-Mungu!
3Mwenyezi-Mungu awabariki kutoka Siyoni;
yeye aliyeumba mbingu na dunia.