Zaburi 119:153-160
Zaburi 119:153-160 BHN
Uangalie mateso yangu, uniokoe, kwa maana sikuisahau sheria yako. Unitetee na kunikomboa; unijalie uhai kama ulivyoahidi. Waovu hawataokolewa kamwe, maana hawajali juu ya masharti yako. Huruma yako ni kubwa, ee Mwenyezi-Mungu, unijalie uhai kama ulivyoahidi. Maadui na wadhalimu wangu ni wengi, lakini mimi sikiuki maamuzi yako. Niwaonapo wahaini hao nachukizwa mno, kwa sababu hawazishiki amri zako. Tazama, ee Mungu, ninavyozipenda kanuni zako! Unijalie uhai kadiri ya fadhili zako. Kitovu cha neno lako ni ukweli, maagizo yako yote adili, yadumu milele.