Parallel
10
Methali za Solomoni
1Hizi ni methali za Solomoni:
Mtoto mwenye hekima ni furaha ya baba yake;
lakini mtoto mpumbavu ni huzuni ya mama yake.
2Mali iliyopatikana kwa njia mbaya haifai,
lakini uadilifu huokoa mtu kutoka kifoni.
3Mwenyezi-Mungu hawaachi waadilifu wapate njaa,
lakini huzipinga tamaa za waovu.
4Uvivu husababisha umaskini,
lakini mkono wa mtu wa bidii hutajirisha.
5Mwenye busara hukusanya wakati wa mavuno,
kulala wakati wa kuvuna ni aibu.
6Mwadilifu hujiletea baraka yeye mwenyewe,
lakini kinywa cha mwovu kimesongwa na ukatili.
7Waadilifu hukumbukwa kwa baraka,
lakini waovu watasahaulika kabisa.
8Mwenye hekima moyoni hutii amri,
lakini mpumbavu aropokaye ataangamia.
9Aishiye kwa unyofu huishi salama,
apotoshaye maisha yake atagunduliwa.
10Akonyezaye kwa nia mbaya huzusha taabu,
lakini aonyaye kwa ujasiri huleta amani.
11Kinywa cha mwadilifu ni chemchemi ya uhai,
lakini kinywa cha mwovu kimesongwa na ukatili.
12 # Taz Yak 5:20; 1Pet 4:8 Chuki huzusha ugomvi,
lakini upendo hufunika makosa yote.
13Kinywani mwa mwenye ufahamu mna hekima,
lakini wasio na akili watachapwa viboko mgongoni.
14Wenye hekima huhifadhi maarifa,
lakini kuropoka kwa mpumbavu huleta maangamizi haraka.
15Mali ya tajiri ndio ngome yake,
umaskini wa maskini humletea maangamizi.
16Tuzo la mtu mwema ni uhai,
lakini mwovu huishia katika dhambi.
17Anayekubali maonyo anaelekea kwenye uhai,
lakini anayekataa kuonywa amepotoka.
18Amchukiaye mwingine kwa siri ni mnafiki,
anayemsingizia mtu ni mpumbavu.
19Penye maneno mengi hapakosekani makosa,
lakini aneyeuzuia ulimi wake ana busara.
20Maneno ya mwadilifu ni kama fedha bora;
akili ya mtu mwovu haina thamani yoyote.
21Maneno ya mwadilifu huwafaa watu wengi,
lakini wapumbavu hufa kwa kukosa akili.
22Baraka za Mwenyezi-Mungu ndizo ziletazo fanaka,
juhudi za mtu haziongezi hapo chochote.#10:22 huzuni … nazo: Au na haongezi hapo huzuni.
23Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo;
lakini watu wenye busara hufurahia hekima.
24Anachoogopa mtu mwovu ndicho kitakachompata,
lakini anachotamani mwadilifu ndicho atakachopewa.
25Kimbunga hupita na mwovu hutoweka,
lakini mwadilifu huimarishwa milele.
26Kama ilivyo siki kwa meno au moshi machoni,
ndivyo alivyo mvivu kwa bwana wake.
27Kumcha Mwenyezi-Mungu hurefusha maisha,
lakini miaka ya waovu itakuwa mifupi.
28Tumaini la mwadilifu huishia kwenye furaha,
lakini tazamio la mwovu huishia patupu.
29Mwenyezi-Mungu ni ngome ya wanyofu,
lakini watendao maovu atawaangamiza.
30Waadilifu kamwe hawataondolewa nchini,
lakini waovu hawatakaa katika nchi.
31Kinywa cha mwadilifu hutoa mambo ya hekima,
lakini ulimi wa mtu mbaya utakatiliwa mbali.
32Midomo ya waadilifu hujua yanayokubalika,
lakini vinywa vya waovu husema tu maovu.