YouVersion Logo
Search Icon

2 Wathesalonike UTANGULIZI

UTANGULIZI
Katika barua hii ya pili ambayo iliandikwa muda mfupi baada ya ile ya kwanza (kati ya mwaka 50 na 51 B.K.), Paulo anazungumzia karibu mambo yaleyale aliyoandika katika barua yake ya kwanza: Tatizo lililozuka kutokana na kufikiria juu ya kuja kwake Kristo. Baadhi ya watu katika jumuiya hiyo hata walidhani kwamba siku yenyewe ya kuja kwake ilikwisha fika (2:2); baadhi waliacha hata kufanya kazi (3:6-12). Madhumuni ya barua hii basi, ilikuwa kusahihisha fikira hizo zisizo sawa katika Kanisa la Thesalonike.
Hali ya Kanisa la Thesalonike haikuwa ya amani hasa tukifikiria maneno kama “jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso mnayopata” (1:4) na “nyinyi mnaoteseka” (1:7). Lakini mtume Paulo anamshukuru Mungu kwa kuwa licha ya hayo mateso, waumini wa Thesalonike wanaendelea kustahimili katika imani na upendo na subira (1:3-4). Uvumilivu wao na kule kubaki imara kutawafanya wapate tuzo wakati Bwana Yesu atakapotokea kutoka mbinguni (1:3-12 na hasa aya ya 6-10). Na, kuhusu kurudi kwake Bwana Yesu Kristo nasi kujiunga naye (2:1), Paulo anasema wazi kwamba kuja huko hakutafanyika sasa hivi. Ni lazima yule “Mwovu” atokee kwanza, lakini Bwana atamwangamiza (2:8).
Katika sura ya 2:13–3:5 Paulo anawapa maneno ya kuwatia moyo na maombi. Mwishoni katika 3:6-15 Paulo anawahimiza waendelee na kazi zao katika jumuiya. Maneno ya Paulo “Asiyefanya kazi, asile” (3:10) yanamtahadharisha msomaji asikubali kupotoshwa na mawazo yanayochanganya imani na fikira zisizo sawa za kutowajibika.

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy