YouVersion Logo
Search Icon

Yohana 1

1
Neno akawa mwili
1 # 1 Yoh 1:1,2; Yn 17:5; Ufu 19:13 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2#Mit 8:22 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3#Kol 1:16,17; Ebr 1:2 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. 4#Yn 5:26 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. 5#Yn 3:19 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
6 # Mt 3:1; Mk 1:4; Lk 3:1-2; 1:13-17,57-80 Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. 7#Lk 3:3 Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. 8#Yn 1:20 Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru. 9Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. 10#Yn 1:3-5 Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. 11Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. 12#Gal 3:26 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13#Yn 3:5,6 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. 14#Isa 7:14; 2 Pet 1:16,17; Isa 60:1; Lk 9:32 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
15 # Yn 1:27,30; Mt 3:11 Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 16#Yn 3:34; Kol 1:19 Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. 17#Rum 6:14; 10:4; Kut 34:6; Zab 25:10; 40:10; 85:10 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. 18#Yn 6:46; 1 Yoh 4:12; Mt 11:27; Lk 10:22; 1 Tim 6:16 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.
Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji
19 # Lk 3:15,16 Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? 20#Mdo 13:25 Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. 21#Kum 18:15,18; Mal 4:5; Mt 17:10; Yn 6:14; 7:40 Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. 22Basi wakamwambia, U nani? Na tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wanenaje juu yako mwenyewe? 23#Isa 40:3; Mt 3:3; Mk 1:3; Lk 3:4 Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya. 24Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo. 25#Mt 21:25 Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule? 26#Mt 3:11; Mk 1:7,8 Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi. 27#Yn 3:26; Mdo 13:25 Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza kamba ya kiatu chake. 28#Mt 3:6,13 Hayo yalifanyika huko Bethania ng'ambo ya Yordani, alikokuwako Yohana akibatiza.
Mwana-kondoo wa Mungu
29 # Yn 1:36; Isa 53:7 Kesho yake alimwona Yesu akija kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30#Yn 15:27 Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 31Wala mimi sikumjua; lakini ili adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nilikuja nikibatiza kwa maji. 32#Mt 3:16; Mk 1:10; Lk 3:22 Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. 33#Lk 3:2; Mt 3:16 Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenituma kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. 34#Mt 3:17 Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.
Wanafunzi wa kwanza wa Yesu
35Tena kesho yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. 36#Yn 1:29; Isa 53:7 Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu! 37Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. 38Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? 39Akawaambia, Njooni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi. 40#Mt 4:18-22 Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu. 41#1 Sam 2:10; Zab 2:2 Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). 42#Mt 16:18; Mk 3:16 Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).
Yesu awaita Filipo na Nathanaeli
43 # Mt 8:22; Mk 2:14 Kesho yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate. 44Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro. 45#Kum 18:18; Isa 7:14; 53:2; Yer 23:5; Eze 34:23 Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. 46#Yn 7:41,52 Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone. 47#Zab 32:2; 73:1; Mwa 25:27 Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. 48Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. 49#2 Sam 7:14; Yn 6:69; Zab 2:7; Mt 14:33; 16:16 Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli. 50Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. 51#Mwa 28:12; Mt 4:11; Mk 1:13 Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.

Currently Selected:

Yohana 1: SRUVDC

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy