YouVersion Logo
Search Icon

Sef 1

1
1 # 2 Tim 3:16; 2 Pet 1:21; 2 Fal 22:1—23:30; 2 Nya 34:1—35:27 Neno la BWANA lililomjia Sefania, mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amaria, mwana wa Hezekia; katika siku za Yosia, mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda.
Hukumu Inayoijia Yuda
2Nitavikomesha kabisa vitu vyote, visionekane juu ya uso wa nchi, asema BWANA. 3Nitamkomesha mwanadamu na mnyama; nitakomesha ndege wa angani, na samaki wa baharini, na hayo makwazo pamoja na wabaya; nami nitamkatilia mbali mwanadamu, asionekane juu ya uso wa nchi, asema BWANA. 4#Hos 10:5Nami nitaunyosha mkono wangu juu ya Yuda, na juu ya watu wote wakaao Yerusalemu; nami nitayakatilia mbali mabaki ya Baali, yasionekane mahali hapa, na hilo jina la Wakemari pamoja na makuhani; 5#1 Fal 11:33na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa BWANA na kuapa pia kwa Malkamu; 6na hao waliorudi nyuma, na kuacha kumfuata BWANA; na hao wasiomtafuta BWANA, wala kumwulizia.
7Nyamaza kimya mbele za Bwana MUNGU;
Kwa maana siku ya BWANA i karibu;
Kwa kuwa BWANA ameweka tayari dhabihu,
Amewatakasa wageni wake.
8Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya BWANA, nitawaadhibu wakuu, na wana wa mfalme, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni. 9Na katika siku ile nitawaadhibu hao wote warukao juu ya kizingiti, waijazao nyumba ya bwana wao udhalimu na udanganyifu. 10#2 Nya 33:14; Neh 3:13Na katika siku ile, asema BWANA kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka milimani. 11#Yak 5:1; Ufu 18:11,12Haya! Lieni, ninyi mkaao katika Makteshi, maana wafanya biashara wote wameangamia; hao wote waliokuwa na mizigo ya fedha wamekatiliwa mbali. 12#Ayu 21:15; Zab 10:11-13Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya. 13#Kum 28:30; Amo 5:11; Mik 6:15Na huko utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao zitakuwa ukiwa; naam, watajenga nyumba, lakini hawatakaa ndani yake; nao watapanda mizabibu, lakini hawatakunywa divai yake.
Siku Kuu ya BWANA
14 # Yer 30:7; Yoe 2:1; Mal 4:5; Ufu 6:17 Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu;
I karibu, nayo inafanya haraka sana;
Naam, sauti ya siku ya BWANA;
Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko!
15Siku ile ni siku ya ghadhabu,
Siku ya fadhaa na dhiki,
Siku ya uharibifu na ukiwa,
Siku ya giza na utusitusi,
Siku ya mawingu na giza kuu,
16 # Yer 4:19; 8:16; Hos 5:8; Amo 3:6 Siku ya tarumbeta na ya kamsa,
Juu ya miji yenye maboma,
Juu ya buruji zilizo ndefu sana.
17Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi. 18#Eze 7:19; Sef 3:8Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha.

Currently Selected:

Sef 1: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy