YouVersion Logo
Search Icon

Yoe 1

1
Maombolezo juu ya Maangamizi ya Nchi
1 # Ebr 1:1; 2 Pet 1:21 Neno la BWANA lililomjia Yoeli, mwana wa Pethueli.
2 # Kum 4:32; Isa 7:17; Dan 12:1; Yoe 2:2; Mt 24:21 Sikieni haya, enyi wazee;
Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi.
Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu,
Au katika siku za baba zenu?
3 # Zab 78:4 Waarifuni watoto wenu habari yake,
Watoto wenu wakawaambie watoto wao,
Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine.
4Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.
5 # Isa 32:10 Levukeni, enyi walevi, mkalie;
Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai;
Kwa sababu ya divai mpya;
Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.
6 # Mit 30:25; Ufu 9:8 Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu,
Lenye nguvu, tena halina hesabu;
Meno yake ni kama meno ya simba,
Naye ana magego ya simba mkubwa.
7 # Isa 5:6 Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.
8 # Isa 22:12; Mit 2:17 Ombolea kama mwanamwali avaaye magunia
Kwa ajili ya mume wa ujana wake.
9 # Yoe 2:14 Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji
Zimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA;
Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.
10 # Yer 12:11; Isa 24:7 Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.
11 # Yer 14:3 Tahayarini, enyi wakulima;
Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu;
Kwa ajili ya ngano na shayiri,
Maana mavuno ya mashamba yamepotea.
12 # Isa 9:3; Yer 48:33; Hos 9:1,2 Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia;
Nao mkomamanga na mtende na mtofaa;
Naam, miti yote ya mashamba imekauka;
Maana furaha imekauka katika wanadamu.
Mwito wa Toba na Sala
13 # Yer 4:8 Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani;
Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu;
Njoni mlale usiku kucha katika magunia,
Enyi wahudumu wa Mungu wangu;
Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji
Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.
14 # 2 Nya 20:3,13 Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini,
Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi;
Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu,
Na kumlilia BWANA,
15 # Yer 30:7; Yoe 2:3; Amo 5:16-18; Isa 13:6 Ole wake siku hii!
Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi. 16#Kum 12:7,12; 16:11Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu? 17Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; ghala zimeachwa ukiwa; mabanda yamevunjika; kwa maana nafaka imekauka. 18#1 Fal 18:5; Hos 4:3Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng’ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya kondoo yamepata mateso.
19Ee BWANA, nakulilia wewe;
Kwa maana moto umeyala malisho ya nyikani,
Na miali ya moto imeteketeza miti yote ya mashamba.
20 # Ayu 38:41; Zab 104:31; 1 Fal 17:7 Naam, wanyama wa mashamba wanakutwetea wewe;
Kwa maana vijito vya maji vimekauka,
Na moto umeyateketeza malisho ya nyikani.

Currently Selected:

Yoe 1: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy