YouVersion Logo
Search Icon

Amo 1

1
1 # 2 Sam 14:2; 2 Fal 15:1-7; 2 Nya 26:1-23; 11:6; Zab 78:70; Hos 1:1; Zek 14:5; 2 Fal 14:23-29 Maneno ya Amosi, aliyekuwa mmoja wa wachungaji wa Tekoa; maono aliyoyaona katika habari za Israeli, siku za Uzia, mfalme wa Yuda, na siku za Yeroboamu, mwana wa Yoashi, mfalme wa Israeli, miaka miwili kabla ya tetemeko la nchi.
Hukumu kwa Jirani za Israeli
2 # Yoe 3:16 Naye alisema,
BWANA atanguruma toka Sayuni,
Atatoa sauti yake toka Yerusalemu;
Na malisho ya wachungaji yataomboleza,
Na kilele cha Karmeli kitanyauka.
3 # Isa 8:4; 2 Fal 10:33; 17:1-3; Yer 49:23-27; Zek 9:1 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Dameski, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameipura Gileadi kwa vyombo vya kupuria vya chuma; 4lakini nitapeleka moto uingie katika nyumba ya Hazaeli, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi. 5#Isa 7:1Nami nitalivunja komeo la Dameski, na kuwakatilia mbali wenyeji wa bondeni mwa Aveni, na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Beth-Adini; na watu wa Shamu watakwenda hali ya kufungwa hata Kiri, asema BWANA.
6 # 2 Nya 28:18; Isa 14:29-31; Yer 47:1-7; Eze 25:15-17; Yoe 3:4-8; Sef 2:4-7; Zek 9:5-7 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waliichukua katika hali ya kufungwa kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu; 7#2 Fal 18:8lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Gaza, nao utayateketeza majumba yake. 8Nami nitamkatilia mbali mwenyeji katika Ashdodi; na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Ashkeloni; nami nitaugeuza mkono wangu uwe juu ya Ekroni; na mabaki ya Wafilisti wataangamia, asema Bwana MUNGU.
9 # Isa 23:1-18; Eze 26:1—28:19; Yoe 3:4-8; Zek 9:1-4; Mt 11:21-22; Lk 10:13-14 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Tiro, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameitia kabila nzima katika mikono ya Edomu, wala hawakulikumbuka agano la udugu; 10lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Tiro, nao utayateketeza majumba yake.
11 # 2 Nya 28:17; Isa 34:5-17; 63:1-6; Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; 35:1-15; Oba 1-14; Mal 1:2-5 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Edomu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, akatupilia mbali huruma zake zote; hasira yake ikararua-rarua daima, akaishika ghadhabu yake milele; 12lakini nitapeleka moto juu ya Temani, nao utayateketeza majumba ya Bosra.
13 # Yer 49:1-6; Eze 21:28-32; 25:1-7; Sef 2:8-11 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya wana wa Amoni, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili wapate kuongeza mipaka yao; 14#Kum 3:11; Eze 25:5lakini nitawasha moto katika ukuta wa Raba, nao utayateketeza majumba yake; pamoja na kupiga kelele siku ya vita, pamoja na tufani katika siku ya chamchela; 15#Yer 49:3na mfalme wao atakwenda utumwani, yeye na wakuu wake wote pamoja, asema BWANA.

Currently Selected:

Amo 1: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy