Luka 16:19, 20, 21, 22, 23, 24, 25, 26, 27, 28, 29, 30, 31
Luka 16:19 NENO
“Palikuwa na mtu mmoja tajiri aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, ambaye aliishi kwa anasa kila siku.
Luka 16:20 NENO
Hapo penye mlango wake aliishi maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima.
Luka 16:21 NENO
Huyo Lazaro alitamani kujishibisha kwa makombo yaliyoanguka kutoka mezani kwa yule tajiri. Hata mbwa walikuwa wakija na kuramba vidonda vyake.
Luka 16:22 NENO
“Wakati ukafika yule maskini akafa, nao malaika wakamchukua akae pamoja na Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa na akazikwa.
Luka 16:23 NENO
Kule Kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa kifuani mwake.
Luka 16:24 NENO
Hivyo yule tajiri akamwita, ‘Baba Ibrahimu, nihurumie na umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake ndani ya maji aupoze ulimi wangu, kwa sababu nina maumivu makuu kwenye moto huu.’
Luka 16:25 NENO
“Lakini Ibrahimu akamjibu, ‘Mwanangu, kumbuka kwamba wakati wa uhai wako ulipata mambo mazuri, lakini Lazaro alipata mambo mabaya. Lakini sasa anafarijiwa hapa na wewe uko katika maumivu makuu.
Luka 16:26 NENO
Zaidi ya hayo, kati yetu na ninyi huko kumewekwa shimo kubwa, ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko wasiweze, wala mtu yeyote asiweze kuvuka kutoka huko kuja kwetu.’
Luka 16:27 NENO
“Akasema, ‘Basi, nakuomba, umtume Lazaro aende nyumbani mwa baba yangu
Luka 16:28 NENO
maana ninao ndugu watano. Awaonye, ili wasije nao wakafika mahali hapa pa mateso.’
Luka 16:29 NENO
“Ibrahimu akamjibu, ‘Ndugu zako wana Maandiko ya Musa na Manabii, wawasikilize hao.’
Luka 16:30 NENO
“Yule tajiri akasema, ‘Hapana, baba Ibrahimu, lakini mtu kutoka kwa wafu akiwaendea, watatubu.’
Luka 16:31 NENO
“Ibrahimu akamwambia, ‘Kama wasipowasikiliza Musa na Manabii, hawataweza kushawishika hata kama mtu akifufuka kutoka kwa wafu.’ ”